Kwanza (sarafu)
Mandhari
Kwanza (kifupi: KZ) ni pesa inayotumika kwa malipo halali katika nchi ya Angola.
Wakati wa uhuru Angola ilirithi pesa ya escudo kutoka Ureno. Mwaka 1977 Kwanza yenye Lwei 100 imeingizwa nchini kama pesa ya kwanza ya kitaifa. Kutokana na kushuka kwa thamani ya fedha mara kwa mara pesa ya Kwanza imebadilishwa mara nne tangu 1977:
- 1977 Kwanza
- 1977 Kwanza Novo (Kwanza Mpya)
- 1995 Kwanza Reajustado (Kwanza iliyosahihishwa)
- 1999 Kwanza (Kwanza Reajustado milioni moja zilibadilishwa kuwa Kwanza mpya 1)
Sarafu za centavos 10 na 50 hazipatikani kwani hazinunui kitu tena.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kwanza (sarafu) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |