Nenda kwa yaliyomo

Kristine Sutherland

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kristine Sutherland

Amezaliwa Kristine Young
17 Aprili 1955 (1955-04-17) (umri 69)
Boise, Idaho, Marekani
Ndoa John Pankow (1986-hadi sasa)

Kristine Sutherland (jina la awali: Kristine Young; amezaliwa Boise, Idaho, 17 Aprili 1955 ni mwigizaji wa filamu na tamthilia kutoka nchini Marekani.

Anafahamika zaidi kwa kucheza uhusika akiwa kama mama mzazi wa Buffy Summers (alicheza kwa jina la Joyce Summers) kwenye mfululizo wa televisheni wa Buffy The Vampire Slayer.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Alibadilisha jina lake kwa vile mara kwa mara alikuwa anachanganywa jina lake na mwigizaji mwingine mwenye jina sawa na lake. Jina lake la mwisho "Sutherland" lilikuwa jina la paka wake, ambaye alimwita jina la "Donald" kutokana na mwigizaji filamu maarufu Donald Sutherland, ambaye, imetokea tu kwa bahati, amecheza awali katika filamu ya Buffy the Vampire Slayer, ambapo lilikuwa jaribio lake la kwanza la Joss Whedon kumleta Buffy katika hali ya wapenzi.[1] Alisoma elimu yake ya juu huko mjini Lexington, Kentucky, ambapo alijisomea masuala ya ugizaji (Tates Creek Drama). Baada ya kuhitimu, akajiunga katika Chuo Kikuu cha Kentucky.

Kristine Sutherland hana uhusiano wowote ule na Donald Sutherland au mtoto wake Kiefer Sutherland.[2]

Uhusika wake wa kwanza kwa Sutherland ulikuwa katika filamu ya Honey, I Shrunk the Kids ya mwaka wa 1989 ambamo alicheza kama Mae Thompson. Mwaka wa 1997, alisailiwa na uhusika wa Joyce Summers kwenye mfululizo wa TV wa Buffy the Vampire Slayer kupitia televisheni ya The WB Television Network. Mtunzi wa tamthilia hiyo Joss Whedon baadaye alitoa sababu zilizomfanya amchague Sutherland kwa uhusika huo kwamba kiukweli alitoka na kijasho chembamba cha kuonesha dalili za kuwa na uwezo wa kucheza uhusika huo.

Vilevile kwa kuwa na imani ya kwamba anafanana na mwigizaji Sarah Michelle Gellar, ambaye alicheza kama binti yake katika tamthilia hiyo. Ameonekana kama muhusika wa kawaida kwenye kipindi hicho katika misimu mitano ya kwanza kabla ya kuondoka, na akarudi tena katika misimu mitatu zaidi, katika msimu wa 1 na 6, 2, na 7 akiwa kama mgeni mwalikwa. Mwezi wa Aprili 2008, alipata uhusika wa ugeni kwenye mfululizo wa New Amsterdam akiwa kama mke wa John Amsterdam, katika kisa cha "Reclassified".

Baada ya kuondoka katika Buffy the Vampire Slayer mnamo 2002, Sutherland ameamua kujiunga na kozi ya masuala ya upigaji picha katika chuo cha Santa Monica College na baadaye kachukua miezi 12 ya makazi-mapumziko huko nchini Italia akiwa na mume wake na binti yake. Alipendezewa na sanaa ya upigaji picha kitu ambacho kimemfanya afungue studio yake mwenyewe.

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Sutherland ameolewa na mwigizaji John Pankow, ambaye kwa sasa anacheza kama "Merc Lapidus" kwenye kipindi cha Episodes. Wana binti mmoja.

Filmografia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]