Nenda kwa yaliyomo

Kolokolo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kolokolo
Kolokolo wa Rudd
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Cisticolidae (Ndege walio na mnasaba na videnenda)
Sundevall, 1872
Ngazi za chini

Jenasi 5:

Kolokolo ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia Cisticolidae. Wanafana na videnenda lakini mkia wao ni mrefu zaidi na wana rangi kali zaidi: kahawia, kijivu au kijani mgongoni na nyeupe, njano na/au nyekundu chini na pengine kichwani na mbawani. Spishi nyingi zina mkufu mweusi kidarini. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara katika misitu na mapori. Hula wadudu. Hulijenga tago lenye kuba ya manyasi, majani na/au vigoga katika kichaka. Jike huyataga mayai 3-5.