Nenda kwa yaliyomo

Zuwakulu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kisigajiru)
Zuwakulu
Zuwakulu domo-kuu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Piciformes (Ndege kama vigong'ota)
Familia: Lybiidae (Ndege walio na mnasaba na zuwakulu)
Jenasi: Buccanodon G.R. Gray, 1855

Gymnobucco Bonaparte, 1850
Lybius Hermann, 1783
Stactolaema C.H.T. Marshall & G.F.L Marshall, 1870
Trachylaemus Reichenow, 1891
Trachyphonus Ranzani, 1821
Tricholaema J. Verreaux & E. Verreaux, 1855

Zuwakulu (pia zuakulu) ni ndege wa familia Lybiidae, lakini spishi za jenasi Pogoniulus zinaitwa vitororo. Spishi zote zinatokea Afrika chini ya Sahara. Ndege hawa ni wanono na wana kichwa kikubwa na domo zito lenye nywele ndefu kuzunguka msingi wake. Spishi nyingi zina rangi kali kama nyekundu na njano. Hula wadudu na aina mpaka 60 za matunda. Spishi kubwa zinaweza kukamata mijusi na vyura. Kwa kawaida dume na jike pamoja huchimba tundu katika tawi au shina lililooza na jike huyataga mayai 2-6 ndani yake. Spishi kadhaa huchimba