Kitororo
Mandhari
(Elekezwa kutoka Pogoniulus)
Kitororo | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Vitororo au kongogolo ni ndege wadogo wa jenasi Pogoniulus katika familia Lybiidae. Ndege hawa ni matoleo madogo ya zuwakulu na mwenendo wao ni takriban sawa na hawa. Vitororo ni ndege wadogo wenye 9-12 cm na 7-15 g. Wana rangi ya kijivu, nyeusi au majani, mistari myeupe na madoa mekundu au njano. Hula wadudu na beri, matini madogo na beri za spishi za kirukia hasa. Dume na jike pamoja huchimba tundu katika tawi au shina lililooza na jike huyataga mayai 2-4 ndani yake.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Pogoniulus atroflavus, Kitororo Kiuno-chekundu (Red-rumped Tinkerbird)
- Pogoniulus bilineatus, Kitororo Kiuno-njano (Yellow-rumped Tinkerbird)
- Pogoniulus chrysoconus, Kitororo Paji-njano Yellow-fronted Tinkerbird)
- Pogoniulus coryphaeus Kitororo-milima (Western Tinkerbird)
- Pogoniulus leucomystax Kitororo Masharubu (Moustached Green-tinkerbird)
- Pogoniulus makawai, Kitororo Kidari-cheupe (White-chested Tinkerbird)
- Pogoniulus pusillus, Kitororo Paji-jekundu (Red-fronted Tinkerbird)
- Pogoniulus scolopaceus Kitororo Kipaku (Speckled Tinkerbird)
- Pogoniulus simplex, Kitororo Kijani (African Green-tinkerbird)
- Pogoniulus subsulphureus, Kitororo Koo-njano (Yellow-throated Tinkerbird)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Kitororo kiuno-chekundu
-
Kitororo kiuno-njano
-
Kitororo paji-njano
-
Kitororo-milima
-
Kitororo koo-njano