Kinyunga (Australia)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kinyunga (au Kinoongar) ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wanyunga katika jimbo la Australia Magharibi. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kinyunga 240. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kinyunga kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi. Wengine huangalia lugha zifuatazo kama lahaja za Kinyunga: Kibibbulman, Kigoreng, Kipinjarup, Kiwajuk na Kiwardandi.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kinyunga (Australia) kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.