Kikope

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jicho la mtu mwenye kikope
Jicho la mtu mwenye kikope

Kikope (Kwa Kiingereza conjunctivitis) ni ugonjwa wa jicho ambao humpata mtu iwapo konjaktiva ya jicho inakuwa nyekundu.

Sababu ya kikope inaweza kuwa maambukizi ya virusi au bakteria. Hivyo tunashauriwa kuosha macho kwa maji safi ya kutitirika.

Ishara na dalili[hariri | hariri chanzo]

Jicho kuwa na rangi nyekundu, uvimbe kwenye konjaktiva, na macho kutoa machozi mengi ni dalili za kawaida kwa aina zote za kikope.

Ugonjwa wa kikope huweza kutambulika kirahisi kwa dalili kama kuwashwa kwa macho na konjaktiva kuwa na rangi nyekundu. Isipokuwa katika aina nyingine za kikope huhitaji vifaa maalum ili kuthibitisha utambuzi.

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kikope kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.