Nenda kwa yaliyomo

Mbayuwayu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kijumbamshale)
Mbayuwayu
Mbayuwayu michirizi mdogo
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Hirundinidae (Ndege walio na mnasaba na mbayuwayu)
Rafinesque, 1815
Ngazi za chini

Jenasi 19:

Mbayuwayu au vijumbamshale ni ndege wa familia Hirundinidae. Spishi nyingine zinaitwa kinega au kizelele. Wanafanana na teleka lakini hawa wamo katika oda yao yenyewe Apodiformes. Mbayuwayu wana miguu mifupi kama teleka lakini mabawa yao ni mafupi zaidi na spishi nyingi zina rangi kama nyekundu, buluu na/au zambarau. Hutua mara kwa mara. Hukamata wadudu wakiruka angani.

Spishi kadhaa huyataga mayai yao ndani ya mashimo asilia au matundu yaliyoachwa na vigong'ota. Spishi nyingi nyingine hulichimba tundu lao katika maada isiyo gumu k.m. ukingo wa mto. Spishi za jenasi Hirundo, Ptyonoprogne, Cecropis, Petrochelidon na Delichon hulijenga tundu lao la matope kupambana na ukuta wa jabali au jengo kwa kawaida karibu na sehemu inayochomoza kama paa la jengo. Jike huyataga mayai 2-5.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine

[hariri | hariri chanzo]