Kijiji cha Makumbusho Daressalaam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kijiji cha Makumbusho)
Jump to navigation Jump to search

Kijiji cha makumbusho mjini Daressalaam ni eneo linalohifadhi mifano ya nyumba na vifaa vya tamaduni mbalimbali zinazopatikana katika nchi ya Tanzania . Eneo hilo lipo katika jiji la Dar es Salaam wilaya ya Kinondoni. Kijiji cha Makumbusho kipo mkabala na barabara ya Ally Hassan Mwinyi nje kidogo ya mji. Kijiji hicho kilianzishwa mwaka 1966 kwa ajili ya kuonyesha na kutunza tamaduni ikiwemo tamaduni za asili , ngoma na tamaduni za makabila mbalimbali kama Wanyakyusa, Makonde, Masai, Chagga, Haya, Ngoni, Yao na mengine mengi.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Kijiji cha Makumbusho