Kichagga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kichagga ni mojawapo ya lugha za Kibantu inayotumiwa na Wachagga, kabila lenye asili katika mkoa wa Kilimanjaro, kaskazini mwa Tanzania.

Watumiaji wanakadiriwa kuwa 2,000,000.

Lugha hiyo inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka unapofika Siha, magharibi mwa mlima Kilimanjaro.

Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika Kirombo (ambacho nacho kinatofautiana kadiri unavyotoka eneo moja hadi jingine; mfano Kisseri, Kimashati, Kimkuu, Kimengwe, Kimahida), Kivunjo, Kimarangu, Kirombo, Kioldimoshi, Kingassa, Kiuru, Kikibosho, Kimachame na Kisiha.

Lugha hizo zinakaribia kufanana kadiri makabila hayo yalivyopakana. Kwa mfano, Kivunjo kinafanana na Kioldimoshi. Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame ambacho pia kinafanana kidogo na Kikibosho.

Baadhi ya Wamachame walihamia sehemu za Meru, Arusha, na kuchanganyikana na Waarusha, hivyo lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Kimeru. Kwa sababu hiyo Wameru wanasikilizana sana na Wamachame ingawa lafudhi zao zinatofautiana kidogo.

Noun project 1822.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kichagga kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.