Kepler (chomboanga)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Artist's impression of the Kepler telescope

Kepler ni chomboanga chenye kazi ya kubeba darubini kilichorushwa angani na taasisi ya NASA (Marekani) kwa shabaha ya kugundua sayari za nje zinazozunguka nyota nje ya mfumo wa jua letu.[1]

Jina lilichaguliwa kwa heshima ya mwanaastronomia Mjerumani wa karne ya 17 Johannes Kepler,[2]

Kepler lilirushwa katika anga la nje mnamo tarehe 7 Machi 2009.[3]

Kazi yake ni kupeleleza sehemu ya Njia nyeupe na kugudua sayari za nje hasa zile ambazo zinazukuka nyota yao kwa umbali penye uwezekano wa kuwa na uhai.[4] [5]

Data zake zinatumwa duniani na kufanyiwa utathmini hapa kwetu.Shabaha ni kutambua nyota zinazoonyesha mabadiliko ya kurudiarudia ya angavu ya nyota zinazosababishwa na sayari zinazopita mbele ya nyota wakati wa kuangaliwa. Yaani kila sayari ikipita nyota yake inapunguza kiasi kiwango cha nuru kinachoonekana na mtazamaji wa nyota hii inaweza kupimwa.[6][7]

Kepler inamaliza kazi[hariri | hariri chanzo]

Kepler ilipaswa kusimamisha kazi yake kwa sababu kulitokea tatizo la kulenga tena darubini pale panapotakiwa na waandisi duniani walishindwa kuondoa tatizo hili. [8]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Kepler Mission. NASA (2009). Iliwekwa mnamo 2009-03-14.
  2. DeVore, Edna. "Closing in on Extrasolar Earths", SPACE.com, 2008. Retrieved on 2009-03-14. 
  3. NASA Staff. Kepler Launch. NASA. Iliwekwa mnamo 2009-09-18.
  4. NASA Staff. Kepler Mission/QuickGuide. NASA. Iliwekwa mnamo 2011-04-20.
  5. AAS Staff. Meeting Program and block schedule. American Astronomical Society. Iliwekwa mnamo 2011-04-20. – click the itinerary builder to get to the abstract of "Kepler planet detection mission: Introduction and first results".
  6. http://www.ustream.tv/recorded/28311736
  7. News (2012). NASA approves Kepler mission extension. kepler.nasa.gov.
  8. Kepler: Nasa retires prolific telescope from planet-hunting duties. BBC News Science & Environment, 2013. [1]