Nenda kwa yaliyomo

Kefee

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

'

Kefee
Kefee
AmezaliwaFebruari 5, 1980
AmefarikiJuni 12, 2014
Kazi yakemwanamke mwimbaji wa Injili na mtunzi kutoka Nigeria


Kefee Obareki Don Momoh (Februari 5, 1980 - Juni 12, 2014), ambaye pia alijulikana kwa jina lake la muziki Kefee, alikuwa mwanamke mwimbaji wa Injili na mtunzi kutoka Nigeria .

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa huko Sapele, Delta mnamo Februari 5, 1980 [1][2]katika familia ya Andrew Obareki ambao wakati huo walikuwa Mashemasi katika kanisa lililoanzishwa na wazazi wa mume wake wa zamani Alec Godwin.

Kefee alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Benin na shahada ya Utawala wa Biashara. Alipokuwa kijana, alijishughulisha kikamilifu na shughuli za kanisa hasa katika kuimba kwaya.[3]

Mapenzi yake ya muziki yalipozidi kukua, alianza kuandika na kutunga nyimbo. Mwaka wa 2000 alitoa albamu iliyoitwa "Trip" na ambayo ilimwezesha kuingia kwenye anga ya muziki ya Nigeria kama msanii wa Injili. Mnamo 2003, alisainiwa na Alec's Entertainment, lebo iliyoanzishwa na mkurugenzi wake wa zamani wa kwaya na alitoa albamu yake ya kwanza ya studio Branama muda mfupi baada ya hapo.

Albamu ya Branama ilimpa mwangaza kama msanii wa Injili aliyekamilika na mauzo ya kitaifa na kimataifa. Branama iliuza kaseti elfu tisa katika wiki tatu na zaidi ya CD/VCD milioni mbili kwa mwezi.[4]

Ilifanya kama sehemu ya mwanzo ya kazi yake ya mafanikio kama msanii wa Injili wa Nigeria. Vibao maarufu vya mwimbaji marehemu ni "Branama" na "Kokoroko"[3]

Alitunukiwa Tuzo ya Balozi mdogo wa Kimataifa wa Amani mwaka wa 2009.[5] Kefee alishinda Tuzo za Headies za 2010 ya Ushirikiano Bora na Timaya kwa "Kokoroko"

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Kefee aliolewa mara mbili. Aliolewa na Alec Godwin kwa miaka mitatu hadi 2008. [6]Aliolewa na mtangazaji wa redio Teddy Esosa Don-Momoh tarehe 3 Machi 2013 huko Sapele, jimbo la Delta.[7][8]

Ingawa chanzo cha kifo kilisemekana kuwa priklampsia, Kefee Obareki Don Momoh alikufa kutokana na kushindwa kwa mapafu katika hospitali ya Los Angeles, California mnamo Juni 12, 2014.[9][10] [11]Alikuwa katika hali ya kukosa fahamu kwa siku kumi na tano.

Alizikwa Ijumaa Julai 11, 2014 katika mji aliozaliwa Okpara Inland, Eneo la Serikali ya Mitaa ya Ethiope Mashariki katika Jimbo la Delta, Nigeria.[12]

Kazi ya muziki

[hariri | hariri chanzo]
Albumu za Studio
  • Branama (2003)
  • Branama 2 (2005)
  • A Piece Of Me (2008)
  • A Chorus Leader (2012)
EPs
  • Dan Maliyo (2012)
Albumu za Posthumous
  • Beautiful (2015)
  1. http://www.premiumtimesng.com/arts-entertainment/164358-kefee-to-be-buried-july-11.html
  2. https://web.archive.org/web/20150707171116/http://www.nigeriafilms.com/news/31413/46/kefee-comes-alive-today-at-her-first-memorial-birt.html
  3. 3.0 3.1 https://web.archive.org/web/20150909110208/http://sunnewsonline.com/new/music-star-kefee-died
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-10-21. Iliwekwa mnamo 2022-05-05.
  5. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-04-16. Iliwekwa mnamo 2022-05-05.
  6. https://web.archive.org/web/20160729200613/http://thenet.ng/2012/01/kefees-ex-husband-alec-godwin-remarries/
  7. https://web.archive.org/web/20160623212429/http://thenet.ng/2012/03/shocking-kefee-weds-star-fms-teddy-esosa/
  8. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-06-10. Iliwekwa mnamo 2022-05-05.
  9. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-07-14. Iliwekwa mnamo 2022-05-05.
  10. http://www.thenigerianvoice.com/news/149521/1/gospel-singer-kefee-is-dead.html
  11. https://web.archive.org/web/20160305082250/http://thenet.ng/2014/06/kefee-dies-after-15-days-in-coma/
  12. http://bellanaija.com/2014/07/12/adieu-kefee-emotional-photos-as-gospel-singer-is-laid-to-rest-in-sapele
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kefee kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.