Nenda kwa yaliyomo

Kayafa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa Giotto kuhusu Yesu mbele ya Kayafa.

Yosefu bin Kayafa (kwa Kiaramu: יוסף בַּר קַיָּפָא, Yosef Bar Kayafa), maarufu kama Kayafa tu (kwa Kigiriki: Καῖάφα) alikuwa kuhani mkuu wa Israeli miaka 18-36). Wakati huo aliendesha kesi ya Yesu akiwa mwenyekiti wa baraza kuu la taifa mjini Yerusalemu.

Kabla ya hapo alihusika na njama ya kumkamata, na baadaye akahusika na jitihada za kumshinikiza liwali Ponsyo Pilato amsulubishe.

Mwaka 1990 karibu na Yerusalemu limepatikana kaburi lenye jina lake.[1].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Jerusalem - Burial Sites and Tombs of the Second Temple Period
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kayafa kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.