Katharine Drexel

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kuingia patakatifu pa Mt. Katharine Drexel huko Bensalem, Pennsylvania, Marekani.

Katharine Marie Drexel (26 Novemba 18583 Machi 1955) alikuwa mtawa wa kike na mwanzilishi wa shirika la Masista wa Ekaristi Takatifu (kwa Kiingereza Sisters of the Blessed Sacrament).

Jumuiya hiyo kwanza ililenga hasa kuwainua Wahindi Wekundu na Wamarekani weusi huko Marekani. Kwa ajili yao alitumia kwa ukarimu na upendo urithi wake mwenyewe.

Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 20 Novemba 1988 na mtakatifu tarehe 1 Oktoba 2000.

Sikukuu yake ni tarehe 3 Machi[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Tarry, Ellen (1958). St. Katharine Drexel - Friend of the Oppressed. New York: Farrar, Straus and Cudahy, Inc.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.