Kahe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kahe ni kata ya Wilaya ya Moshi Vijijini katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 19,142 [1] walioishi humo. Msimbo wa posta ni 25230.

Kahe ni eneo lilikutanisha jamii za kutoka Old Moshi, Arusha Chini na Milima ya Upare. Makabila yanayopatikana Kahe ni kama Wakahe, Wamasai, Wapare na Waarusha na Wameru. Aliyekuwa kiongozi wa kimila alijulikana kama Mangi Maya na badae Mangi Mangoto ambae alitawala eneo zima la Kahe. Kwa upande wa Magharibi Kahe inapakana na kiwanda maarufu cha sukari cha TPC. Hivyo baadhi ya wakazi wake wananufaika na uwekezaji huu kwa kuajiriwa kiwandani hapo.

Kahe ni maarufu mkoani Kilimanjaro kwa kilimo cha mpunga na mbogamboga kwani eneo lake lina wingi wa maji unaoruhusu kilimo kipindi chote cha mwaka. Kahe ambayo ilikuwa maarufu kwa biashara kutokana na kukutanisha reli ile inayotoka nchi jirani ya Kenya na ile inayotoka Dar es Salaam kupitia Tanga uchumi wake uliathiriwa na kufa kwa reli hiyo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]


Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Moshi Vijijini - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Arusha Chini | Kahe | Kahe Mashariki | Kibosho Kati | Kibosho Magharibi | Kibosho Mashariki | Kilema Kaskazini | Kilema Kati | Kilema Kusini | Kimochi | Kindi | Kirima | Kirua Vunjo Magharibi | Kirua Vunjo Mashariki | Kirua Vunjo Kusini | Mabogini | Makuyuni | Mamba Kaskazini | Mamba Kusini | Marangu Magharibi | Marangu Mashariki | Mbokomu | Mwika Kaskazini | Mwika Kusini | Okaoni | Old Moshi Magharibi | Old Moshi Mashariki | Uru Kaskazini | Uru Kusini | Uru Mashariki | Uru Shimbwe


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kahe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.