Kadriye Gökçek

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kadriye Gökçek alikuwa mwamuzi wa mpira wa miguu, na mtumishi wa serikali wa Uturuki. [1] Alioorodheshwa kwenye orodha ya waamuzi wanawake na FIFA tangu 2008.

Kazi ya uamuzi[hariri | hariri chanzo]

Kadriye Gökçek alianza kazi yake ya uamuzi kama mwamuzi msaidizi mnamo Agosti 10 1996, katika Ligi ya A2 . Baada ya kutumikia mwaka mmoja na nusu kama mwamuzi msaidizi katika Ligi ya TFF ya daraja la Tatu nchini Uturuki, alifuzu kuchezesha mechi kama mwamuzi wa ligi hiyo mnamo Januari 17, 1999. Tangu wakati huo, anachezesha katika viwango mbalimbali vya mashindano. [2]

Mnamo 2008, Gökçek alifuzu kuchukua beji ya FIFA . [3] Alichezesha mechi katika kundi la 8 la mashindano ya UEFA ya Wanawake chini ya miaka 19 2010 raundi ya kwanza ya mchujo iliyofanyika Hungaria mnamo 2009. [4]

Aliwahi kuwa mwamuzi katika mzunguko wa kwanza wa mashindano ya kufuzu mashindano kombe la UEFA chini miaka 17 mwaka 2011 huko Ireland Kaskazini. [5]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Referee Details - Kadriye Gökçek". Türkiye Futbol Federasyonu. Iliwekwa mnamo 2013-10-14. 
  2. "Referee Details - Kadriye Gökçek". Türkiye Futbol Federasyonu. Iliwekwa mnamo 2013-10-14. "Referee Details - Kadriye Gökçek". Türkiye Futbol Federasyonu. Retrieved 2013-10-14.
  3. "Gündemden kısa kısa...". Retrieved on 2013-10-14. 
  4. "Kadriye Gökçek’e UEFA’dan görev". Retrieved on 2013-10-14. 
  5. "UEFA'dan Kadriye Gökçek'e Görev". Retrieved on 2013-10-14. Archived from the original on 2016-03-03. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kadriye Gökçek kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.