Nenda kwa yaliyomo

Jukwaa la watazamaji vijana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jukwaa la Watazamaji Vijana ni tawi la sanaa ya uigizaji ambalo linajumuisha aina zote za majukwaa ya michezo yanayohudhuriwa ama kuundwa kwa ajili ya hadhira kwa vijana. Inahusisha aina tofauti tofauti za mbinu na maonyesho ya kumbi za michezo, ikiwa ni pamoja na michezo, ngoma, muziki, vibonzo, sarakasi, majukwaa ya michezo, na mengine mengi. Jukwaa hili huwa na michezo tofauti tofauti ambayo huchezwa ulimwenguni kote, inachukua aina nyingi ya michezo ya kitamaduni na isiyo za kitamaduni, na inachunguza mada anuwai kuanzia hadithi za hadithi hadi unyanyasaji wa wazazi.

Tawi hili lilianzishwa katika karne ya 20, na ni tawi la hivi karibuni la Sanaa ya Maonesho. Nchini Marekani mara nyingi huzingatia kutoa burudani, ingawa mizizi yake ipo sana katika elimu. Waandishi wengi na makampuni ya uzalishaji wameanza kuhudumia watazamaji wa Jukwaa hili, na kusababisha ongezeko la mara kwa mara la nyenzo za maonyesho kwa watoto. Katika siku hizi, makampuni au vikundi vya uzalishaji katika kumbi hizi vinaweza kupatikana katika maeneo mengi ya Marekani na duniani kote.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Jukwaa hili lilianza kutumiwa kwa upande wa watoto miaka mingi iliyopita na kutajwa kwa mara ya kwanza ni katika kumbukumbu ya Madame de Genlis ingizo la 1784, ambapo alikuwa anaelezea utendaji wa binti zake wawili kwenye onesho la Duke Chartres. Jukwaa hili likawa tawi lake la majukwaa ya michezo katika karne ya 20, ilionekana kwa mara ya kwanza huko Moscow wakati mwigizaji wa Kirusi Natalia Satz kuanzisha Jukwaa la Watoto wa Moscow mwaka 1918. Katika hatua zake za awali, jukwaa la Watoto wa Moscow liliona lengo lake kama kuwakilisha mahitaji ya watoto, kutenganisha mapambano ya utotoni na yale ya maisha ya watu wazima. Vikundi sawia vya Jukwaa la watazamaji vijana vilianzishwa nchini Uingereza, Marekani, Ufaransa, na Czechoslovakia kati ya Vita vya Kwanza vya Kidunia na Vita vya Pili vya Dunia.

Jukwaa la Watazamaji Vijana Marekani

[hariri | hariri chanzo]

Elimu ndio ilikuwa lengo kuu la kuanzisha jukwaa hili pindi ilipofika marekani. Mnamo mwaka 1903, Alice Minnie Herts alianzisha jukwaa la Elimu la watoto ambalo ndilo lilikuwa jukwaa la kwanza Marekani kutoa kazi za maonyesho pamoja na watoto .Ijapokuwa jukwaa hilo halikudumu lakini lilikuwa kama chachu ya uanzishwaji wa makupuni mengine nchini, halikadhalika kwenye ukuaji wa uandishi na uzalishaji wa kazi za sanaa kwa vijana.