Judy Jay

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Judy Mahlatji (alizaliwa Desemba 2, 2001)[1], ni Dj kutoka Afrika kusini na mtayarishaji wa rekodi, anayejulikana kama Judy Jay.[2]Mnamo Novemba 2021 aliachana na muziki kutokana na matatizo ya afya ya akili[3][4][5], baada ya kukaa miezi miwili mbali na sanaa alitangaza kurudi mapema mwaka 2022[6][7][8].

Baada ya kurejea kwenye muziki, alipokea muongozo wa tamasha ulio na matukio 37 yanayoendelea mpaka mwishoni mwa Juni, na matukio nje ya nchi. Atatembelea nchi jirani kama vile Lesotho, Eswatini na Botswana mtawalia[9].

Katikati ya mwaka 2021, Judy Jay alishinda Diesel Denim Friday[10], ambapo alikua anashindana na zaidi ya madj 70 nchini. Aliletwa kwenye shindano hilo na HERO DJ, Lamiez Holworthy[11].

Mabishano[hariri | hariri chanzo]

Wasanii wengi huona aibu kutokana na historia zao au walikotoka, Judy ni miongoni mwa wasanii hao. Mashabiki na wafuasi walisikitishwa sana Judy alipohojiwa kwenye Channel O ambapo aliulizwa anaishi wapi na akasema Bolivia estate huko Polokwane ambapo wafuasi wake walidhani angetaja Ga-Sekhukhune kama sehemu alikotoka hata hivyo, cha kusikitisha hakupataja.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Judy Jay – Biography, Age, Career & Net Worth". SA Online Portal (kwa en-US). 2022-03-08. Iliwekwa mnamo 2022-04-24. 
  2. "Judy Jay – Biography, Age, Career & Net Worth". SA Online Portal (kwa en-US). 2022-03-08. Iliwekwa mnamo 2022-04-24. 
  3. Thobile Mazibuko. "Judy Jay hangs up her headphones, quits being a DJ". www.iol.co.za (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-24. 
  4. https://www.kaya959.co.za/judy-jay-shares-the-reason-she-quit-music-in-2021-and-announces-comeback/
  5. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-02-11. Iliwekwa mnamo 2022-04-24. 
  6. Oluthando Keteyi. "Judy Jay to return after quitting being a DJ". www.iol.co.za (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-24. 
  7. By Andiswa Ngenyane. "JUDY JAY’S BACK MONTHS AFTER QUITTING!". Dailysun (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2022-04-24. 
  8. "Judy Jay 2023 & 2022 Latest Songs Download, Mixtape, EP, Video and Album - tunes". ZAtunes (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2023-02-26. 
  9. https://www.amapiano.co/za/judy-jay-gets-massive-bookings-hours-after-she-announced-her-return/
  10. "ICYMI: Judy Jay Takes The Diesel Denim Friday Win". Online Youth Magazine | Zkhiphani.com (kwa en-US). 2021-06-09. Iliwekwa mnamo 2022-04-24. 
  11. Thobile Mazibuko. "Judy Jay wins Diesel Denim Friday". www.iol.co.za (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-24.