Joyce Blessing

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Joyce Blessing ni mwanamuziki wa nyimbo za Injili kutoka Ghana[1].

Maisha ya awali na elimu[hariri | hariri chanzo]

Joyce Akosua Twene anayejulikana kama Joyce Blessing alizaliwa na Christopher Kwabena Twene na Gladys Yaa Kyewaa tarehe 15 Mei huko Accra, Ghana. Joyce ni mtoto wa nne kwa wazazi wake. Alikulia na ndugu wengine ambao wote walilelewa na mama yao huko Kumasi, Mkoa wa Ashanti nchini Ghana ambako alisoma shule ya msingi.

Kazi ya muziki[hariri | hariri chanzo]

Joyce alikuwa akipenda sana muziki na hivyo alianza kuimba kanisani akiwa na umri wa miaka 14 na pia alihakikisha kuwa hakosi tamasha za muziki zilizofanyika karibu naye alipokuwa mdogo hata mama yake alipojaribu kumzuia kuhudhuria sherehe hizo. .

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "FLASHBACK: 'I used to weed people’s gardens to get money for my music' – Joyce Blessing". GhanaWeb (kwa Kiingereza). 2022-07-21. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-02-26. Iliwekwa mnamo 2023-02-26. 
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Joyce Blessing kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.