Nenda kwa yaliyomo

John Njue

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kardinali John Njue

John Njue ni askofu wa kanisa katoliki nchini Kenya aliyekuwa askofu mkuu wa Nairobi tangu 6 Oktoba 2007. Siku chache baada ya kuwa askofu mkuu aliteuliwa na Papa Benedikto XVI kuwa kardinali.

Njue alizaliwa mwaka 1944 katika kijiji cha Kiriari (Embu). Alisoma shule ya Gituri Primary na Sekondari.

Baada ya kumaliza shule mwaka 1966 aliendelea kusoma theolojia na kumaliza kwenye Chuo Kikuu cha Urbaniana mjini Roma kwa MA ya falsafa.

Tar. 6 Januari 1973 alipadrishwa huko Embu na kuwa kasisi wa parokia ya Kariakomu (Meru) 1974. 1978 akawa mwalimu kwenye seminari ya upadre ya St. Augustine mjini Bungoma.

1986 aliteuliwa kuwa askofu wa dayosisi ya Embu. Kati ya 1987 na 1991 akawa mwenyekiti wa kamati za maendeleo na huduma za jamii , pia ya kamati ya haki na amani chini ya Ofisi Kuu ya Wakatoliki Kenya.

Mwaka 2002 akawa askofu mkuu msaidizi wa dayosisi kuu ya Nyeri. Baada ya kuondoka kwa askofu mkuu Raphael S. Ndingi Mwana a'Nzeki aliyehamishwa Nairobi alishika nafasi ya Askofu Mkuu.

Mwaka 2007 alimfuata Mwana a'Nzeki katika nafasi ya askofu mkuu wa Nairobi. Njue ni kardinali ya pili nchini Kenya baada ya marehemu Maurice Otunga.