Jiriwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
A Jiriwa ya kufunga mezani, B jiriwa ya mashine, C kibanio cha mkononi.

Jiriwa (kwa Kiingereza: vise au vice) ni kibanio cha chuma au mbao ambacho hushikilia vitu kwa imara wakati vinapofanyiwa kazi.

Huwa na mikono miwili, mmoja uliosanikishwa na mwingine unaoweza kusogezwa kwa njia ya parafujo ya kukaza au wenzo wa kubana.

Kilango (vali) kikishikwa katika jiriwa ndogo.

Aina tofauti[hariri | hariri chanzo]

Jiriwa ya seremala[hariri | hariri chanzo]

Jiriwa ya seremala yenye mikono ya mbao.

Jiriwa huunganishwa katika meza ya seremala, kwa kawaida sawa na uso wa meza. Mikono yake ni ama ya mbao ama ya chuma; kama ni chuma kinafunikwa kwa mbao ili kutoacha alama kwenye vipande vinavyoshikwa.[1]

Jiriwa ya fundi vyuma[hariri | hariri chanzo]

Jiriwa ya fundi vyuma hutengenezwa kwa chuma cha pua.

Jiriwa ya fundi vyuma hutumiwa kushika metali, si mbao, wakati wa kukata au kupiga tupa.

Jiriwa hiyo kwa kawaida hufungwa kwa skrubu juu ya uso wa meza ya fundi. Mara nyingi huwa na sehemu ndogo ya fuawe. Kwa kawaida hukaa juu ya kiti chenye mhimili wa kuzunguka kinachorahisisha kufanya kazi pande zote.

Jiriwa ya fundi bomba[hariri | hariri chanzo]

Fundi bomba huhitaji jiriwa yenye mikono inayoshika bomba kirahisi, wakati anapokata hesi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Bentzley, Craig (2011). "Installing a Bench Vise". Woodcraft Magazine (June/July): 50–53. http://www.woodcraftmagazine.com/onlineextras/41-Vises.pdf.
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.