Nenda kwa yaliyomo

Jimmy Cliff

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jimmy Cliff

Jimmy Cliff ni mwanamuziki wa Jamaika. Amezaliwa 1 Aprili 1948 huko St Catherine, Jamaika. Jina lake la kuzaliwa ni James Chambers. Hasa anapiga muziki wa Reggae. Tangu mwaka wa 1968 alitoa vibao vingi. Mwaka wa 2004 alitoa kibao cha Black Magic.

Alirekodi wimbo wake wa kwanza akiwa ana miaka kumi pekee. Wimbo huo ulikwenda kwa jina la "Hurricane Hattie." Ukiwa mkono wa mtayarishaji maarufu Leslie Kong. Kitendo ambacho kilipelekea kusogea katika ramani ya muziki wa Jamaika. Ushirika wao haukushia katika kibao cha kwanza bali pia hata vibao vya usoni katika karia ya muziki wake. Ambapo kwa pamoja walitoa "Miss Jamaica" na "King of Kings."

Katika kujitafuta, mwishoni mwa miaka ya 1960 alihamia nchini Uingereza. Akiwa huko, akasaini mkataba na lebo ya Island Records. Tangu hapo mvua ya albamu za kimataifa ikaanza kunyesha. Albamu ya kwanza kimataifa litoka mnamo mwaka wa 1967 ikiwa na jina la "Hard Road to Travel". Ikafuatiwa na "Wonderful World, Beautiful People" (1969). Ndani yake kukiwa na wimbo wa "Vietnam." Wimbo pendwa nyakati hizo.


Mwaka wa1972, Jimmy Cliff akapanda ngazi. Aliingia rasmi katika angala la filamu. Akatupia nyago kama muhusika mkuu katika filamu ya "The Harder They Come." Ikiwa imetayarishwa na Perry Henzell. Ikachukuliwa kama kioo cha kutazama harakati za kijaana anayejitafuta kupitia muziki wa reggae. Vibwagizo vyake ni pamoja na wimbo wa "The Harder They Come," "You Can Get It If You Really Want," na "Many Rivers to Cross." Ambapo ngoma hizo zilisukuma kutambulika kwa muziki wa reggae ulimwenguni kote.


Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jimmy Cliff kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.