Nenda kwa yaliyomo

Jimbo la Mataifa ya Kusini, Ethiopia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Jimbo la Makabila ya kusini)

Jimbo la Mataifa ya Kusini (kwa Kiamhari: ደቡብ ብሔሮች ብሔረሰቦችና ሕዝቦች, Ye-Debub Bəheročč Bəheresebočč-ənna Həzbočč; kwa Kiingereza "Southern Nations, Nationalities, and Peoples’ Region", kifupi: SNNPR) ni moja kati ya majimbo 12 ya kujitawala ya Ethiopia.

Jimbo liko kusini mwa nchi, likipakana na Kenya upande wa kusini, Sudan Kusini upande wa magharibi na majimbo ya Ethiopia ya Gambela upande wa kaskazini na Oromia upande wa kaskazini, mashariki na kusini-mashariki.

Tofauti na majimbo mengine ya Ethiopia yenye kabila au kundi 1 hasa, hapa kuna vikundi vingi vidogovidogo kwa jumla 45. Wakazi wengi huishi mashambani ama vijijini au kama wahamiaji katika makambi yao ya kuhama.

Mji mkuu wa jimbo ni Awassa, lakini baada ya jimbo kumegwa, mji huo umekuwa wa jimbo la Sidama, hivyo unafikiriwa mwingine.

 
Majimbo ya Ethiopia
Bandera ya Ethiopia
Addis Abeba | Afar | Amhara | Benishangul-Gumuz | Dire Dawa | Gambela | Harar | Oromia | Sidama | Somali | Mataifa ya Kusini | Tigray