Nenda kwa yaliyomo

Jedwan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Mokhtar Jedwan
Picha ya Mokhtar Jedwan

Mokhtar Jedwan, pia huandikwa Jedwane, au Jedouan (Kwa Kiarabu : المختار جدوان, Rabat, 1967) ni mwimbaji wa Morocco, ambaye aliacha kazi ya uimbaji mwaka 2008 na akawa mhubiri wa Kiislamu na msomaji wa Kurani .

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Mokhtar Jedwan alikulia katika familia ya wasanii, ambapo kila mmoja kati ya kaka zake watatu alikuwa na kikundi chake cha muziki. Alishawishiwa hasa na kusikiliza vikundi vya Nass El Ghiwane na Jil Jilala .

Mwishoni mwa 1983, Jedwane aliunda okestra yake mwenyewe na akaanza kuimba katika hafla maalumu na sherehe hadi alipogunduliwa na mtayarishaji ambaye alimpa mkataba wa kufanya nae kazi. [1] Tangu wakati huo, ametoa albamu kadhaa na kuwa mwanamuziki anayejulikana sana nchini Morocco.

Mnamo 2008, akiwa na umri wa miaka arobaini, Jedwan aliamua kuacha kazi yake ya muziki, na kujitolea wakati wake kwa mahubiri ya Kiislamu. [2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]