Ivan Zaytsev

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Ivan Zaytsev

Ivan Zaytsev (amezaliwa 2 Oktoba 1988) ni mchezaji wa mpira wa wavu wa Italia mwenye asili ya Urusi.

Ivan Zaytsev ni mwanachama wa timu ya taifa ya mpira wa wavu ya Italia na klabu ya Italia ya Modena Volley.

Alizawadiwa medali ya shaba katika michezo ya Olimpiki huko London mwaka 2012, medali ya fedha ya mashindano ya Ulaya (2011, 2013), medali ya shaba katika michuano ya Dunia (2013, 2014).

Pia alikuwa bingwa wa mpira wa wavu huko Italia mwaka 2014 na alizawadiwa medali ya fedha katika Michezo ya Olimpiki Rio mwaka 2016.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Ivan Zaytsev ni mtoto wa mchezaji wa michezo ya Olimpiki ya mpira wa wavu, Vyachelav Zaytsev. Alizaliwa huko Spoleto, Italia ambapo baba yake alikuwa akicheza wakati huo. Mama yake, Irina Pozdnyakova, alikuwa mwogeleaji maarufu wa zamani.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

LegaVolley Serie A profile player Archived 9 Agosti 2009 at the Wayback Machine.