Nenda kwa yaliyomo

Ironman Triathlon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kuogelea ni moja wapo ya mchezo wa Ironman Triathlon
Kuendesha baiskeli ni moja wapo ya mchezo wa Ironman Triathlon
Kukimbia ni mojawapo ya mchezo wa Ironman Triathlon

Ironman Triathlon ni aina ya mchezo inayopangwa na World Triathlon Corporation (WTC) na inahusu kuoegelea kwa maili 2.4, kuendesha baiskeli kwa maili 112 na kukimbia kwa maili 26.22 mfualulizo bila kupumua wala kusimama. Ironman Triathlon yasemekana kuwa ndiyo mbio ngumu zaidi duniani.

Michezo hii huwa imetengewa masaa kumi na sita au kumi na saba na kwa kawaida huanza saa moja asubuhi. Kuogelea huisha saa tatu na dakika ishirini asubuhi, kuendesha baiskeli hufungwa saa kumi na moja unusu jioni huku kukimbia kukiisha saa sita usiku. Anayeweza kumaliza maili zote kwa wakati uliotengwa huibuka kuwa Ironman.

Wachezaji hufanya mazoezi magumu ili waweze kumudu michezo hii na kuibuka washindi.

Historia ya Ironman Triathlon[hariri | hariri chanzo]

Michezo hii ya Ironman Triathlon ilianza baada ya michezo ya Oahu Perimeter Relay mwaka 1977 ambako kulizuka mjadala kuhusu ni wanaspoti gani wanaweza kuogelea vizuri zaidi, kuendesha baiskeli kwa kasi sana na kwenda mbio zaidi.

Ironman World Championship[hariri | hariri chanzo]

Michezo hii imekuwa maarufu sana, hivi kwamba kuna kombe la dunia la mabingwa wa Ironman Triathlon. Ili kushiriki katika Ironman World Championship, washiriki hufanya mazoezi makali na kuhitimu kushiriki baada ya kupewa pointi kutoka vitengo vya chini.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Ironman Triathlon kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.