Nenda kwa yaliyomo

Immaculate Akello

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

mmaculate Akello (aliyezaliwa 1996) ni mjasiriamali wa kijamii , mwanaharakati wa mabadiliko ya hali ya hewa, mwanaharakati wa haki za binadamu na mwanasheriawa Uganda ambaye lengo lake kuu ni kubadilisha maisha ya wanawake wa vijijini kaskazini mwa Uganda. [1] Akello ndiye mwanzilishi wa Generation Engage Network, shirika linaloongozwa na vijana ambalo linaangazia haki za mazingira na demokrasia ya mazingira Kaskazini na Kati mwa Uganda. Kupitia shirika hili, aliwakilisha Uganda katika Bunge la Vijjana mwaka wa 2018 jijini Arusha, Tanzania na alikuwa spika wa mkutano wa vijana wa Bunge la Kitaifa la 2018 nchini Uganda. [1] [2]

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Akello alisomea Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala alihitimu Mei 2019. [3]

Wakati wake katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Akello alikuwa Mbunge wa Sheria, pia alikuwa mwakilishi wa Watu Wenye Ulemavu kwenye Muungano wa Chama. [4] Akolle alifanya kazi na Kituo cha Uchambuzi wa Sera (CEPA) shirika lisilo la faida ambalo linatetea demokrasia ya Bunge chini ya bunge la Uganda. [5] Lengo lake kuu lilikuwa juu ya utawala na demokrasia pamoja na haki za wakimbizi nchini Uganda. [4] Baada ya mwezi wa kufanya kazi na CEPA, aliitwa kufanya kazi na Umoja wa Mataifa kwa mkataba wa miezi ambayo uliongezwa hadi Desemba 2019.

  1. 1.0 1.1 "Immaculate Akello – Akina Mama wa Afrika" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-04-26.
  2. "I am Generation Equality: Immaculate Akello, climate change activist and lawyer standing up for rural women". UN Women – Headquarters (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-25.
  3. KIU. ".:: Alumni Voice: Immaculate Akello | Kampala International University, Uganda". kiu.ac.ug (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-25.
  4. 4.0 4.1 KIU. ".:: Alumni Voice: Immaculate Akello | Kampala International University, Uganda". kiu.ac.ug (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-25.
  5. "IMMACULATE AKELLO – CEDA" (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-09-18. Iliwekwa mnamo 2022-04-26.