Nenda kwa yaliyomo

Idris Elba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

== Idris Elba

Idris Elba
Amezaliwa6 Septemba 1972 (51)
UraiaUingereza
Kazi yakeMwigizaji
NdoaSabrina Dhowre Elba (n. 2019)
Watoto2

==

Idris Elba ni mwigizaji wa Uingereza. Yeye alizaliwa tarehe 6 septemba mwaka wa 1972 katika mji wa London. Yeye ni mtoto pekee ya Winston na Eve Elba. Baba yake anatoka nchi ya Sierra Leone na mama yake anatoka nchi ya Ghana[1]. Yeye ana watoto wawili, Isan (mkubwa) na Winston (mdogo) Elba. Yeye alikuwa na Isan, binti yake, na mke wake wa zamani yake Hanne Norgaard na alikuwa na Winston na mpenzi wa zamani wake Naiyana Garth. Katika mwaka wa 2019 yeye aliolewa mwanamitindo Sabrina Dhowre. [2][3]

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Wakati alipokuwa mtoto yeye daima alikuwa na shauku ya kufanya kazi katika ulimwengu wa sanaa ya maonyesho. Kwa hivyo, yeye alicheza michezo ya muziki wakati alipokuwa mwanafunzi. Katika mwaka wa 1990 yeye alipata ufadhili kushughulikia National Youth Music Theatre katika mji wa London. Pia, wakati alipokuwa mwanafunzi na alikuwa mshiriki wa National Youth Music Theatre yeye alikuwa diskojoka; yeye alitumia jina Big Dris [1][4]. National Youth Music Theatre ilimsababisha kugeukia uigizaji rasmi. Kwa mfano, katika miaka ya tisini yeye alicheza maonyesho ya televisheni mengi kama 2Point 4Children, Absolutely Fabulous, The Ruth Rendell Mysteries, Insiders, na Dangerfield. Mwishoni yeye alicheza katika mayonyesho ya televesheni na filamu za Uingereza lakini baada yake alihamia nchi ya Marekani katika miaka ya tisini, kisha maisha yake yalianza kubadilika upesi. Mwishoni yeye aliishi katika umaskini lakini kwa bahati katika mwaka wa 2002 yeye alianza kuingia tasnia ya filamu ya Marekani. Kwa mfano, yeye alicheza uhusika wa “Stringer Bell” katika maonyesho ya televisheni “The Wire” kwa misimu mitatu. Baada ya yeye alicheza “The Wire” yeye aligeuka kuwa mwigizaji maarufu katika nchi ya Marekani[1][2]. Hususani ulimwengu wa burudani ya watu weusi wa Amerika kama “Daddy’s Little Girls”, “Obsessed” na Beyonce, na “American Gangster” na Denzel Washington[1][2].

Idris ni mtu mwelekevu kwa sababu yeye alicheza katika video za muziki chache ambazo yeye alifanya rap. Katika mwaka wa 2019, yeye alicheza video “Boasty” na Stefflon Don, Sean Paul, na Wiley. Yeye alikuwa na mashairi ambayo yeye alifanya rap kwa chini ya dakika moja[2]. Pia, yeye alikuwa dijei wa harusi ya mwana mfalme Harry na Meghan Markle katika mwaka wa 2018 na sikukuu ya Coachella katika mwaka wa 2019 [2][5]. Katika mji wa London yeye ana biashara ya rekodi inaitwa “7Wallace”. Biashara ya rekodi yake illitwa jina la msanii maarufu ya rap Christopher Wallace au Biggie Smalls[2].

Pia, Idris ni mwigizaji ambaye alicheza aina tofauti za filamu. Kwa mfano, yeye alicheza katika filamu za sayansi ya ubunifu kama “Prometheus”, filamu za vitendo kama mfululizo ya Thor, na filamu za uhai kama "Zootopia"[2][6]. Kwa sababu yeye alicheza katika filamu nyingi tofauti, yeye anachuma marupurupu katika mwigizaji ya “A-List”. Pia, wakati yeye alicheza katika filamu yoyote ilikuwa na mafanikio kuleta pesa nyingi[4]. Yeye alipata na kupendekezwa dhidi ya tuzo za filamu. Idris Elba alipendekezwa na alipata tuzo nyingi. Kwa mfano, tuzo za Guild, tuzo za Primetime Emmy, tuzo za NAACP, na tuzo za BAFTA. Kwa tuzo za Guild yeye alipata tuzo kwa utendaji bora kama mwigizaji msaidizi kwa filamu "Beasts of no Nation" katika mwaka wa 2015. Pia, yeye aliptata tuzo ya Guild kwa utendaji bora kama mwigizaji wa kiume katika tamthilia ya televisheni katika mwaka wa 2015 kwa tamthilia ya televisheni “Luther”. Na Pendezeko, yeye alipata pendezeko tatu za tuzo za Emmy kwa tamthilia ya televisheni “Luther” kama bora mwigizaji wa mkuu na mgeni kwa miaka ya 2011 na 2012[7]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "Idris Elba | Biography, TV Shows, Movies, & Facts | Britannica". www.britannica.com (kwa Kiingereza). 2024-04-16. Iliwekwa mnamo 2024-04-18.
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 "Idris Elba - Movies, Spouse & Age". Biography (kwa American English). 2020-10-21. Iliwekwa mnamo 2024-04-18.
  3. "Idris Elba's 2 Kids: All About Isan and Winston". Peoplemag (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-18.
  4. 4.0 4.1 "Idris Elba | Rotten Tomatoes". www.rottentomatoes.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-18.
  5. Condé Nast (2019-02-27). "Idris Elba Explains How He Got the D.J.-ing Gig for Harry and Meghan's Wedding". Vanity Fair (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-04-18.
  6. "When Idris Elba said playing Heimdall in Thor movies was 'torture'". The Indian Express (kwa Kiingereza). 2021-07-31. Iliwekwa mnamo 2024-04-18.
  7. "Idris Elba". TVGuide.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-18.

https://www.biography.com/actors/idris-elba

https://www.tvguide.com/celebrities/idris-elba/bio/3000385554/

https://www.rottentomatoes.com/celebrity/idris_elba

https://www.britannica.com/biography/Idris-Elba

https://www.vanityfair.com/style/2019/02/idris-elba-dj-prince-harry-meghan-markle-wedding

https://indianexpress.com/article/entertainment/hollywood/when-idris-elba-described-playing-heimdall-in-thor-movies-as-torture-7431876/

https://people.com/all-about-idris-elba-kids-7497590#:~:text=Sophie%20Dodd%20is%20a%20freelance,PEOPLE%20from%202018%20to%202022.&text=Idris%20Elba%20is%20a%20proud,with%20ex%2Dgirlfriend%20Naiyana%20Garth