Denzel Washington

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Denzel Washington mwaka 2018

Denzel Hayes Washington Jr. (alizaliwa Desemba 28, 1954) ni mwigizaji na mtengenezaji wa filamu wa Marekani. Amekuwa akizungumziwa sana kama mwigizaji ambaye alirekebisha upya "dhana ya nyota wa sinema ya kawaida" na hivyo kuleta dhana ya kwamba nyota katika filamu anaweza akawa mtu tu wa kawaida lakini mwenye fani na ujuzi tofauti na vile alivyochukuliwa katika jamii.[1]

Katika kipindi chake chote cha kazi kwa zaidi ya miongo minne, Washington amepokea tuzo nyingi, zikiwa ni pamoja na tuzo ya Tony, tuzo mbili za Akademi, tuzo tatu za Golden Globe na Silver Bears mbili.[2] Mnamo 2016, alipokea Tuzo ya Mafanikio katika Maisha ya Cecil B. DeMille, na mnamo 2020, The New York Times alimtaja mwigizaji bora wa karne ya 21.[3] Mnamo 2022, Washington alipokea nishani ya rais ya Uhuru aliyopewa na Rais Joe Biden.[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Denzel Washington kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.