Ibrahima Konaté
Ibrahima Konaté (alizaliwa Paris[1], 25 Mei 1999[2]) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa kulipwa kutokea nchini Ufaransa ambaye anacheza kama beki wa kati katika klabu ya Liverpool F.C. inayoshiriki Ligi Kuu Uingereza (EPL) na timu ya taifa ya Ufaransa. Akianzia na klabu Sochaux, Konaté alihamia RB Leipzig mwaka 2017. Baada ya miaka minne na klabu hiyo, Liverpool ilimsajili mwaka 2021 kwa ada ya paundi milioni 36. Alishinda kombe la EFL na kombe la FA katika msimu wake wa kwanza.
Maisha yake[hariri | hariri chanzo]
Ibrahima Konaté[3] alikulia Paris na ni mtoto wa pili kutoka mwisho kati ya watoto wanane waliozaliwa na wazazi kutoka Mali.[4][5] Ni muislamu.[6]Ukiachana na soka, Konaté ni shabiki wa filamu ya katuni ya anime namanga, na kutaja mfululizo wa filamu ya Attack on Titan kama mfululizo wake anaoupenda zaidi.[7]
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ "Ibrahima Konaté". (fr)
- ↑ Ibrahima Konaté: Overview. ESPN.
- ↑ Squad List: FIFA World Cup Qatar 2022: France (FRA). FIFA (18 December 2022).
- ↑ Ibrahima Konaté: 'The final in Paris, my home. I couldn't have dreamed it'. The Guardian (26 May 2022).
- ↑ Touré, Noyine (7 February 2019). Ibrahima Konaté affole l'Europe.
- ↑ Hendrix, Hale (5 April 2020). Ibrahima Konate Childhood Story Plus Untold Biography Facts.
- ↑ Northcroft, Jonathan. "Ibrahima Konaté: I asked Jürgen Klopp, 'If I was your son, what would you advise?", 27 May 2022.
![]() |
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ibrahima Konaté kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |