Nenda kwa yaliyomo

Hospitali ya Huruma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hospitali ya Huruma ni mojawapo kati ya hospitali tatu zinazomilikiwa na Jimbo Katoliki la Moshi na ni hospitali inayohudumia (CDH) Wilaya ya Rombo.

Ilianza kama hospitali ya Kanisa mnamo mwaka 1968. Iko katika kijiji cha Ibukoni wilaya ya Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro, kaskazini mashariki mwa Tanzania, umbali wa km 80 kutoka manispaa ya Moshi na mita 100 kutoka makao makuu ya Halmashauri ya Rombo.[1]

Kuna zahanati 7 katika jimbo katoliki na hospitali moja ya wakala wa hiari ambayo iko chini ya uangalizi wa hospitali hiyo. Kutokana na eneo la kijiografia inapopatikana, hospitali hiyo husaidia kuhudumia wagonjwa kutoka nchi jirani ya Kenya hususani kutoka Rombo Masai, Chumvini, Njukini, Taveta, Loitoktoki na wagonjwa pia kutoka Moshi Vijijini na Wilaya ya Monduli.

Kwa miaka 7 iliyopita Serikali ilikuwa na uwezo wa kusaidia tu katika masuala ya kipengee cha Emolument ya kibinafsi na malipo mengineyo (OC) ambayo haikuwa inatosha kubeba huduma za hospitali, lakini kuanzishwa kwa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kumewezesha wagonjwa wengi kupata huduma za kiafya kiurahisi ikilinganishwa na hapo awali.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. About us Ilihifadhiwa 29 Januari 2020 kwenye Wayback Machine., tovuti rasmi ya Huruma Hospital