Horatius

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Sanamu ya Horasi mjini Verona

Quintus Horatius Flaccus (pia: Horasi; 8 Desemba 65 KK - 27 Novemba 8 KK) alikuwa mshairi mashuhuri wa Roma ya Kale.

Alizaliwa kama mtoto wa mtumwa aliyepewa uhuru na bwana wake na kutajirika baadaye. Hivyo aliweza kumpa mwanawe elimu nzuri. Alisoma Roma na baadaye Ugiriki.

Aliandika mengi kwa lugha ya Kilatini akasifiwa wakati wake na katika karne zilizofuata.

Kati ya maneno yake yaliyorudiwa mara kwa mara ni:

  • Sapere aude! - "Thubutu kujua" (yaani: Ujiamini kutumia akili !)
  • Dulce et decorum est pro patria mori - "Ni tamu tena inafaa kufa kwa nchi yako."
  • Carpe diem - "Shika siku" (yaani: usipoteze nafasi za siku ya leo)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]