Holly Bradshaw
Mandhari
Holly Bethan Bradshaw (née Bleasdale, alizaliwa Novemba 2, 1991)[1] ni mwanariadha Mwingereza aliyejikita katika kuruka nguzo.[2]
Kwa sasa anashikilia rekodi Uingereza kwenye mashindano ya ndani na nje, akiweza kuruka mita 4.87 (mashindano ya ndani mwaka 2012) na mita 4.90 (mashindano ya nje mwaka 2021). Bradshaw alishinda medali ya shaba katika michuano ya Olimpiki majira ya joto mwaka 2020. Pia alishinda medali ya shaba kwenye michuano ya ndani ya dunia mwaka 2012, medali ya dhahabu kwenye michuano ya ndani ya ubingwa Ulaya mwaka 2013, medali ya shaba kwenye michuano ya ubingwa Ulaya mwaka 2018, na medali ya fedha kwenye michuano ya ndani ya ubingwa Ulaya mwaka 2019.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://teamengland.org/team-england-athletes/holly-bradshaw. Imeongezwa mnamo 03.12.2021
- ↑ http://news.bbc.co.uk/sport2/hi/athletics/16670397.stm. imeongezwa mnamo 03.12.2021