Hifadhi ya Taifa ya Borena
Hifadhi ya Taifa ya Borena, ni mbuga ya taifa iliyopo kusini mwa Ethiopia . Hifadhi ya taifa hiyo ilianzishwa mwaka 2017 na ni mojawapo ya maeneo makubwa zaidi ya hifadhi nchini Ethiopia. [1]
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Hifadhi ya taifa ya Borena iko kusini mwa Ethiopia. Inachukua eneo la kilomita za mraba 45,366. Hifadhi hii iko kwenye ukingo wa kusini wa Nyanda za Juu za Ethiopia . Imepakana upande wa kusini na mpaka wa Kenya na Ethiopia. Inapakana na Hifadhi ya wanyamapori ya Chelbi upande wa magharibi, na Hifadhi ya Wanyamapori ya Yabelo upande wa kaskazini.
Ikolojia
[hariri | hariri chanzo]Sehemu kubwa ya mbuga hii imefunikwa na vichaka na nyanda za nyasi, sehemu ya misitu ya Somalia ya Acacia–Commiphora. [2]
Mimea
[hariri | hariri chanzo]Mazingira ya misitu ya milima ya Ethiopia yanaenea hadi sehemu ya kaskazini ya hifadhi hiyo na inajumuisha misitu ya Afromontane, misitu ya savanna. [2]
Wanyama
[hariri | hariri chanzo]Mbuga ya taifa ya Borena ina angalau aina 40 spishi za mamalia ambao ni pamoja na pundamilia wa Burchell, pundamilia wa Grevy, mbweha wenye mgongo mweusi, Beisa oryxes, gerenuks, Warthogs, na swala wa Grant . [3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Nigatu, Tesfaye. (2016). POTENTIALITY ASSESSMENT FOR ECOTOURISM DEVELOPMENT IN DIDA HARA CONSERVATION SITE OF BORENA NATIONAL PARK, ETHIOPIA. International Journal of Tourism & Hospitality Reviews. 3. 45. 10.18510/ijthr.2016.314.
- ↑ 2.0 2.1 "Borena". DOPA Explorer. Accessed 3 March 2022.
- ↑ Jarso Qanchoro. https://www.academia.edu/45110374/Factors_Influencing_of_Pastoralist_Perceptions_towards_Wildlife_Conservation_in_Borana_National_Park_Southern_Ethiopia. Factors Influencing of Pastoralist Perceptions towards Wildlife Conservation in Borana National Park, Southern, Ethiopia. (Arba Minch University, Bale-Robe, Ethiopia, 2020). Accessed May 31, 2022.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Borena kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |