Herode Agripa
Mandhari
(Elekezwa kutoka Herode Agripa I)
'Herode Agripa, kwa Kigiriki 'Ἡρώδης Ἀγρίππας, Herodes Agrippas, (10 KK – 44 BK), alikuwa mfalme wa sehemu kubwa ya Palestina katika karne ya 1 kutoka ukoo wa Herode Mkuu, babu yake .
Baba yake alikuwa Aristobulo IV na mama yake Berenike.[1]
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Marcus Julius Agrippa, ambalo alipewa kwa heshima ya mwanasiasa wa Roma Marcus Vipsanius Agrippa.
Alianza kutawala mwaka 41 BK.
Ndiye anayesemwa katika Matendo ya Mitume (Agano Jipya, Biblia ya Kikristo), hasa kama muuaji wa Yakobo Mkubwa muda mfupi kabla hajafa mwenyewe.
Kumbe mwandishi wa Kiyahudi Yosefu Flavio anamsifu na kumuita "Agripa Mkuu".[2]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Mason, Charles Peter (1867), "Agrippa, Herodes I", katika Smith, William (mhr.), Dictionary of Greek and Roman Biography and Mythology, juz. la 1, Boston: Little, Brown and Company, ku. 77–78, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-05-22, iliwekwa mnamo 2013-12-17
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ Josephus, Antiquitates Judaicae xvii. 2. § 2
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Yohanan Aharoni & Michael Avi-Yonah, "The MacMillan Bible Atlas", Revised Edition, p. 156 (1968 & 1977, by Carta Ltd.).
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Jewish Encyclopedia: Agrippa I.
- Agrippa I, article in historical sourcebook by Mahlon H. Smith
- Sergey E. Rysev. Herod and Agrippa Archived 19 Juni 2008 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Herode Agripa kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |