Nenda kwa yaliyomo

Herbert Grönemeyer

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Herbert Grönemeyer
Herbert Grönemeyer, 2004
Herbert Grönemeyer, 2004
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Herbert Arthur Wiglev Clamor Grönemeyer
Amezaliwa 12 Aprili 1956 (1956-04-12) (umri 68)
Asili yake Göttingen, Lower Saxony, Ujerumani
Aina ya muziki Rock, Pop, Soft rock
Kazi yake Mwimbaji, Mwigizaji, Mtunzi
Miaka ya kazi 1978–1988, 1990–mpaka sasa
Studio EMI, Co.KG
Ame/Wameshirikiana na Pop 2000
Tovuti http://www.groenemeyer.de/


Herbert Arthur Wiglev Clamor Grönemeyer (amezaliwa tar. 12 Aprili 1956) ni mwigizaji na mwanamuziki maarufu kutoka nchini Ujerumani. Anafahamika sana kwa nchi ya Ujerumani, Austria na Switzerland. Amecheza kama mwandishi wa habari wa vita Lieutenant Werner kwenye filamu ya Wolfgang Petersen Das Boot, lakini baadaye akazingatia zaidi shughuli zake za kimuziki. Albamu yake ya tano inaitwa 4630 Bochum (1984) na albamu yake ya ishirini inaitwa Mensch (Binadamu) (2002) ni rekodi za lugha ya Kijerumani zilizouza vizuri kwa muda wote.

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Grönemeyer mara nyingi huelezea asili ya maisha yake binfasi kwamba yamelala katika mji wa Kijerumani wa Bochum ambapo ametumia maisha yake ya utotoni kwa kiasi kikubwa, ujana na utu uzima wa awali. Hadi leo, wimbo wa Bochum, aliutoa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1984, ni moja kati ya nyimbo za alama yake, hasa wakati anatumbuiza kwenye makumbi. Kuzaliwa kwake mjini Göttingen na sio mjini Bochum ana maelezo yake mwenyewe: "Nimezaliwa mjini Göttingen tu kwa sababu mama yangu alikuwa akizimia mara kwa mara wakati ana ujauzito wangu. Amefanya hivi kila mara amejigeuza upande wake wa kushoto, na hakuna hata mmoja aliyemwamini. Mjini Göttingen kulikwa na profesa, mtaalamu, naye hakumwamini vilevile, kwa kilele hicho kalala chini, kazimia, na kuniletea mimi kwenye ulimwengu huu. Hii ndiyo sababu nimezaliza mjini Göttingen."

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Albamu[hariri | hariri chanzo]

 • 1978 — Ocean Orchestra
 • 1979 — Grönemeyer
 • 1980 — Zwo
 • 1982 — Total egal
 • 1983 — Gemischte Gefühle
 • 1984 — Bochum
 • 1986 — Sprünge
 • 1988 — Ö
 • 1988 — What's all this
 • 1990 — Luxus
 • 1991 — Luxus (English)
 • 1992 — So gut
 • 1993 — Chaos
 • 1994 — Cosmic Chaos
 • 1995 — Unplugged
 • 1995 — Live
 • 1996 — Chaos (English)
 • 1998 — Bleibt alles anders
 • 2000 — Stand der Dinge (Double DVD/CD)
 • 2002 — Mensch
 • 2003 — Mensch live (Double DVD)
 • 2006 — "Zeit, dass sich was dreht" / "Celebrate the day" (Official 2006 FIFA World Cup Anthem) (Maxi CD)
 • 2007 — 12
 • 2008 — Was muss muss

Filmografia[hariri | hariri chanzo]

 • 1976 — Die Geisel (imeongozwa na Peter Zadek)
 • 1978 — Von Tag zu Tag (imeongozwa Ulrich Stein)
 • 1978 — Uns reicht das nicht (imeongozwa na Juergen Flimm)
 • 1979 — Daheim unter Fremden (imeongozwa na Peter Keglevic)
 • 1981 — Das Boot (imeongozwa na Wolfgang Petersen)
 • 1982 — Doktor Faustus (imeongozwa na Franz Seitz)
 • 1982 — Frühlingssinfonie (imeongozwa na Peter Schamoni)
 • 1984 — Die ewigen Gefühle (imeongozwa na Peter Beauvais)
 • 1985 — Väter und Söhne (imeongozwa na Bernhard Sinkel)
 • 2007 — Control (imeongozwa Anton Corbijn)
 • 2010 — The American (imeongozwa na Anton Corbijn)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons