Nenda kwa yaliyomo

Henry Wanyoike

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Joseph Kibunja & Henry Wanyoike in Hong Kong, 2008

Henry Wanyoike (alizaliwa 1974) ni Mwanariadha wa Kenya aliye Kipofu. Anashiriki katika mashindano ya Paralympics katika shindano la Marathon.

Kazi yake

[hariri | hariri chanzo]

Wanyoike ni mmoja wa Wanariadha wa kasi sana duniani. Alianza kukimbia akiwa mtoto na tayari alikuwa na ndoto ya kujiunga na kundi la Kenya la wanariadha, nchi ambayo inajulikana kwa kuwakuza Wanariadha wengi wa Massafa marefu wa Kimataifa kuliko nchi nyingine yoyote.

Alitia fora katika mita 5000 na mita 10,000.

Mnamo 1995, Wanyoike alikuwa kipofu wakati alipata mshtuko. Alisimulia, "Nilienda kitandani nikiwa mzima, kuamka nikaamka kwa giza". Usiku huo alipoteza karibu asilimia 95 ya uwezo wake wa kuona na polepole akiupoteza wote. "Nilifikiria maisha yangu yamefikia kikomo",[1] anasimulia.

Mamaye Grace alimchukua katika kliniki ya macho ya Kikuyu[2], (Hospitali ya karibu ya macho inayodhminiwa na shirika la [[Christian Blind Mission International]], CBMI), inayotambulika kama moja ya vituo bora zaidi vya watu walio na shida ya macho katika eneo la Afrika Mashariki.

Petra Verweyen, msimamizi wa mradi wa Low Vision alimsaidia kujipanga tena kimaisha na akampanga kujifunza kushona fulana. Kwa shukrani kubwa alikubali mradi huo na kuahidi kuwasaidia vipofu wengine kujitegemea kimaisha , vile amefanya.

Baada ya kushinda Nishani ya Dhahabu kule Sydney, Australia katika Mashindano ya Paralympic ya 2000, Wanyoike amenunua mashine nyingi za kushona kutokana na zawadi ya fedha alizokabidhiwa na watu maarufu kama vile Arnold Schwarzenegger. Saa hii yeye ni mwajili wa watu wengine vipofu wa Kenya na kuwafunza kufuma fulana.

Kiongozi Wake

[hariri | hariri chanzo]

Mwanariadha kopofu huwa na mtu wa kumwongoza aliyefunganishwa naye mkononi. Kiongozi hutumia kiunganishi hiki kumwashiria mwanariadha, bila kumzidi kasi, wakati wa kugeuka, kupunguza kasi na kuhepa kizuizi, iwe kiwanjani au barabarani. Henry alipozoea kushirikiana na viongoza, alichipuka haraka kama mwanariadha kipofu wa kimataifa.

Hili lilimpatia nafasi katika kikundi cha Kenya cha kuwakilisha Kenya katika mashindano ya Sydney ya Paralympics ya 2000 katika shindano la mita 5000.

Tatizo lililoibuka ni kuwa viongozi wake hawangestahimili kasi yake. Hata hivyo, licha ya kushinda medali ya Dhahabu katika mashindano ya Paralympics, aliweka pia rekodi mpya ya Paralympics. Sasa hivi Wanyoike hukimbia na Kiongozi wake na rafiki taangu utoto, Joseph Kibunja.

Mashindano Anayoyashiriki

[hariri | hariri chanzo]

Kinyume na washindani wengi ambao huboresha ujuzi wao katika shindano moja, Henry ni mmoja wa wale ambao wamejiboresha katika mashindano mengi. Katika miaka 10 iliyopita, ameshiriki katika mashindano ya Half-Marathon, mbio za barabarani za kilomita 10, mita 5,000 na mita 1,500. Anashikilia rekodi ya Dunia ya Marathon kwa vipofu ya 2:31:31 aliyoiweka jijini Hamburg mnamo 2005.

Mafanikio

[hariri | hariri chanzo]
Henry Wanyoike na Kiongozi wake wakati wa Paralympics jijini Athens
Henry Wanyoike na Kiongozi wake wakati wa Paralympics jijini Athens
  • Desemba 2007: Nafasi ya 8 kwa ujumla katika Singapore half-marathon (1:25:15)
  • Novemba 2006: Nafasi ya 121 katika mashindano ya New York Marathon (2:40:14) - Washiriki 38,368
  • Aprili 2006: Nafasi ya 5 katika mashindano ya Bonn

half-marathon (1:14:44) - washiriki 2,675

  • Februari 2006: wa 6 katika mashindano ya Hong Kong

half-marathon (1:16:47) - Washiriki 9000

(2:52) - washiriki 177 pekee kati 3000 walimaliza kwa wakati (saa 5)

half-marathon (1:16:07)

  • Oktoba 2005: wa 3 kwa mashindano ya TUI half-marathon

mjini Palma, Mallorca (1:15:24)

  • Septemba 2005: Mshindi katika mashindano ya half-marathon

mjini Wetzlar (01:14:41)

  • Mei 2005: wa 3,kwa takribani washiriki 4500

katika mashindano ya half-marathon ya Hannover (1:11:25)

  • Aprili 2005 (24 Aprili): Rekodi mpya ya Dunia mjini

Hamburg: 2:31:31

  • Aprili 2005 (17 Aprili): Rekodi mpya ya Dunia jijini

London: 2:32:51

  • Septemba 2004: Nishani ya Dhahabu na rekodi mpya

ya Dunia katika mashindano ya 5,000 m (15:11.07) na 10,000 m (31:37.25) jijini Athens

  • Mei 2004: Boston, mudawa kasi zaidi katika shindano la Marathon (2:33:20)
  • Februari 2004: Hong Kong, mshindi na rekodi mpya ya Dunia

ya shindano lahalf marathon (1:10:26)

  • Desemba 2003: Singapore, shaba katika shindano la mbio za barabarani, akikimbia zaidi ya mita 5,000

katika umbali wa zaidi ya mita 1500

  • Agosti 2003: Canada, dhahabu katika mashindano ya mita 5,000

na 10,000

(2:49:03)

  • Oktoba 2002: Mshindi wa Kombe la Boston katika mashindano ya barabarani ya Mita 5,000
  • Julai 2002: Lille: dhahabu mbili na

rekodi ya Dunia ya mita 5,000 (15:17.75) na mita 10,000 (32:34.31)

  • Aprili 2002: rekodi ya Dunia na dhahabu katika mashindano ya

vipofu ya marathon ya Japan

  • Januari 2002: Jijini Cairo: medali mbili za dhahabu

katika mashindano ya mita 800 na 1500, Fedha katika shindano la mita 400

  • 2000: Mashindano ya Paralympics ya Sydney: Mshindi na Medali yake ya kwanza ya dhahabu katika shindano la mita

5,000 (15:46.29)

Virejeleo

[hariri | hariri chanzo]
  1. World record holder to run in Jersey Marathon Ilihifadhiwa 10 Novemba 2012 kwenye Wayback Machine. BBC, accessed 07/11/07
  2. Kuhusu Henry Wanyoike: Paralympics.org Ilihifadhiwa 29 Mei 2010 kwenye Wayback Machine.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]