Hellen Kijo Bisimba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search


Hellen Kijo Bisimba
Alizaliwa 10 Oktoba 1954
Nchi Tanzania
Kazi yake Alikuwa mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu Tanzania.
Watoto wanne

Hellen Kijo Bisimba (alizaliwa mkoani Kilimanjaro, 10 Oktoba 1954) alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Center - LHRC) kuanzia mwaka 1996 hadi 2018.

Elimu yake[hariri | hariri chanzo]

Alisoma Korogwe, Tanga. Ana watoto wanne.

Dr. Hellen Kijo Bisimba amesoma shahada ya uzamivu ya sheria katika chuo kikuu (daktari wa falsafa) Warwick Uingereza. Mnamo waka 2018 Dr. Hellen alipata cheti cha kutambuliwa na ubalozi wa marekani nchini Tanzania kama ni mwanamke wa kwanza nchini Tanzania kupigania haki za binadamu baada ya kusimama na kutoa tamko dhidi ya serikali juu ya mauaji yaliyofanyika visiwani Zanzibar kwa waandamanaji yaliyo tokea mwaka 2001.[1] [2]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Amefanya kazi katika shirikia la LHRC kwa muda wa miaka 18 akiwa kama mkurugenzi katika shirika hilo.

Dhamira yake ya kupigania na kuhamasisha haki za binaadamu ilianza miaka ya sabini 70’s akiwa bado ni mwanafunzi wa sekondari kidato cha tano na sita mkoa wa Tanga, hii ni mara baada ya kugoma kuandika barua ya maelezo kwa mkuu wa shule iliyopelekea kusimamishwa masomo yake kwa muda.

Kitendo hiki kilimfanya awe mstari wa mbele kupigania haki za binaadamu kwa miaka takribani arobaini sasa.

Dr.Hellen kijo Bisimba amestaafu kazi tangu Agosti 2018.


Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hellen Kijo Bisimba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.