Nenda kwa yaliyomo

Harry Maguire

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Harry Maguire, alizaliwa 5 Machi 1993 ni mchezaji wa soka wa Uingereza, ambaye anacheza kama beki wa kati katika klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza ambayo ni Manchester United F.C. na timu ya Taifa ya Uingereza.

Alizaliwa Sheffield, alikuja kupitia klabu ya vijana ya Sheffield United kabla ya kuhitimu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo mwaka 2011.

Harry Maguire

Alicheza michezo 166 ya kitaaluma katika klabu ya Blades na alikuwa Mchezaji wao wa Mwaka mara tatu mfululizo. Alihamishia Hull City kwa £ 2.5 milioni, ambaye alicheza kwa mkopo Wigan Athletic mwaka 2015. Alijiunga na Leicester City mwaka 2017 kwa ada ya £ milioni 17.

Baada ya hapo amejiunga na Manchester United F.C. mwaka 2019.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Harry Maguire kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.