Haka
Haka ni aina mbalimbali za ngoma za sherehe katika utamaduni wa Wamaori wa New Zealand. Ngoma hizi ni sanaa ya uigizaji zinazotumbuizwa kwa pamoja kwa miondoko ya nguvu, kukanyaga miguu kwa mdundo, na kuongozwa na sauti. Kihistoria, haka hufanywa na wanaume na wanawake kwa hafla za kijamii kama kukaribisha wageni, kusherehekea mafanikio, au katika mazishi. Pia, vikundi vya shule vinatumbuiza pia haka, na shindano kubwa la sanaa hii, Te Matatini, hufanyika kila baada ya miaka miwili[1].
Haka imejulikana kimataifa hasa kupitia timu za michezo za New Zealand, kama All Blacks, ambazo hutumbuiza haka kabla ya mechi kama njia ya kuonyesha changamoto kwa wapinzani. Hata hivyo, dhana kwamba haka ni michezo ya vita pekee imepingwa na wasomi wa Kimaori, ambao wanasisitiza kuwa maana yake ni pana zaidi.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Haka | English meaning". Oxford Advanced Learner's Dictionary (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 25 Juni 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Haka kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |