Nenda kwa yaliyomo

Habari Leo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Habari Leo
Jina la gazeti Habari Leo
Lilianzishwa 2006
Eneo la kuchapishwa Dar es Salaam
Nchi Tanzania
Mwanzilishi Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania (TSN)
Mhariri Tuma Abdullah
Mmiliki Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mchapishaji Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania (TSN)
Makao Makuu ya kampuni Dar es Salaam
Tovuti https://habarileo.co.tz/

Habari Leo ni gazeti la kila siku linalotolewa kwa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania. Ni gazeti mojawapo linaloandikwa kwa Kiswahili lenye wasomaji wengi nchini humo.

Gazeti hilo ni mali ya kampuni ya serikali ya Tanzania "Tanzania Standard (Newspapers) Limited". Kwa mujibu wa tovuti ya serikali, gazeti la Habari Leo ni moja kati ya magazeti manne ya serikali ambalo lilianzishwa rasmi 21 Desemba, 2006 ili kusaidia gazeti la Kiingereza la Daily News katika kutoa elimu, taarifa na kuwa sehemu muhimu ya mawasiliano ya serikali kwa wananchi na pia wananchi kwa serikali.

Mwaka 2016 Habari Leo liliadhimisha miaka 10 ya kuanzishwa kwake.

Magazeti dada[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Sanga, A. N. (2018). Mkengeuko wa ujumi wa kiafrika katika hadithi fupi andishi za kiswahili kipindi cha utandawazi: Mifano kutoka magazeti ya Habari Leo, Nipashe na Mwananchi (Doctoral dissertation, Chuo Kikuu cha Dodoma).

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]