Nenda kwa yaliyomo

Hanoi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Hà Nội)
Hanoi - Hà Nội

Barabara Le Thai To mjini Hanoi
Habari za kimsingi
Mkoa Hanoi
Anwani ya kijiografia 21°2'N, 105°51'E
Kimo 18 m juu ya UB
Eneo 921 km²
Wakazi 3.083.800 (2004)
Msongamano wa watu watu 3.348 kwa km²
Simu 84 (nchi), 4 (mji)
Mahali

Hanoi (Kivietnam: Hà Nội; "mji kati ya mito") ni mji mkuu wa Vietnam mwenye wakazi zaidi ya milioni 3.

Mji uko kando ya Mto Mwekundu katika delta ya mto huu takriban km 60 kabla ya mdomo wake.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kati ya 1945 hadi 1976 ilikuwa mji mkuu wa Vietnam ya Kaskazini. Iliwahi kuwa mji mkuu wa sehemu kubwa ya Vietnam kati ya karne ya 11 hadi 1802 hadi uhamisho wa Kaisari kwenda Hue.

1873 Hanoi ilivamiwa na Ufaransa ikawa makao makuu ya makoloni yake ya Indochina iliyounganisha Vietnam na Kambodia. Muundo wa mji wa leo umetokana na utawala wa Wafaransa waliopanga barabara pana na nyofu na mpango wa miraba lakini walibomoa sehemu kubwa ya mji wa kale.

Kati ya 1940 hadi 1945 Hanoi ilitawaliwa na Japani iliyoshiriki na utawala wa Kifaransa.

Tar. 2 Septemba 1945 rief Ho Chi Minh alitangaza mjini hanoi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Vietnam. Cheo cha mji mkuu wa nchi kikarudishwa kutoka Hue kuja Hanoi.

Kati 1946 hadi 1954 mji uliona mapigano makali ya Wafaransa na jeshi la ukombozi wa Viet Minh. Wakati wa vita ya Marekani katika Vietnam Hanoi iliona uharibifu kutokana na mabomu ya Marekani. Krismasi ya 1872 tani 40,000 za baruti zilitupwa Hanoi.

Tangu muungano wa Vietnam, Hanoi imekuwa mji mkuu wa nchi yote.

Leo hii Hanoi ni mji wa viwanda ikiwa na nafasi ya pili baada ya mji wa Ho Chi Minh (Saigon) ulioko kusini mwa nchi hiyo. Kuna viwanda vya machine, kemia, nguo na bidhaa za ubao.

Picha za Hanoi

[hariri | hariri chanzo]


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hanoi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.