Guillermo Moreno (mwanasiasa wa Argentina)
Guillermo Moreno ni mwanasiasa wa Argentina (Chama cha Justicialist) aliyefanya kazi kama Katibu wa Biashara ya Ndani katika serikali ya Rais Cristina Fernández de Kirchner. Ni mmoja wa wafuasi wakuu wa Kirchnerism.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Moreno, mara nyingi, anajulikana kama "the cowboy" kutokana na mbinu zake za ukali katika kushughulika na makampuni na wanasiasa. Akawa na sifa mbaya, miongoni mwa wakurugenzi wa kampuni za Argentina, kwa kutishia kwa uwazi kutumia vurugu na kwa kutoa bastola katika mikutano katika ofisi yake.
Yeye, pia, alikuwa akishutumiwa na taifa zima kwa kujaribu kuingilia kati katika shirika la INDEC,taasisi ya takwimu rasmi, akiwafuta kazi maafisa waliokataa kudanganya hasa kuhusu mfumuko wa bei.
Moreno alikuwa mwanachama wa bidii nyingi wa kundi la vijana la Peronist,tawi la maandamano ya Kiperonisti lililopendekeza serikali ya kijamii kama ile ya mapinduzi ya Cuba, katika miaka ya 1970.
Cheo chake cha kwanza katika serikali kilikuwa Katibu wa Uzalishaji katika serikali ya jiji la Buenos Aires, akifanya kazi chini ya meya Carlos Grosso,katika miaka ya mwanzo wa mwongo wa 1990. Baadaye, alikuwa naibu wa Katibu wa Biashara katika urais wa Eduardo Duhalde (2002-2003).
Moreno alikuwa rafiki wa Néstor Kirchner kabla Kirchner akuwe rais katika mwaka wa 2003. Yeye alikuwa mmoja wa wanachama wa Kundi la Calafate, kundi la kufikiria mikakati na mipango mbalimbali lililoundwa na Néstor Kirchner mwenyewe kama mbinu ya kuzalisha njia tofauti za kuendeleza sera za miaka ya 1990.
Katika serikali ya Néstor Kirchner, Moreno alifanya kazi kama Katibu wa Mawasiliano,cheo alichohudumia kwa miaka miwili kabla ya kuchukua kiti cha Katibu wa Biashara ya Ndani. Cheo alichopewa baada ya Néstor Kirchner kustaafu na mke wake Cristina Fernández de Kirchner kuwa rais mnamo 10 Desemba 2007.
Moreno amesemekana kuwa kiongozi wa kimabavu, asiyefanya kazi vizuri na asiyeweza kazi aliyopewa. Imesemekana kuwa ana ushawishi mkubwa katika siasa ya taifa zaidi ya unaofaa unapoangalia cheo chake kiko chini cha Waziri wa Uchumi. Inaaminika kuwa mapambano yake na Waziri wa zamani Martin Lousteau ndiyo yaliosababisha kujiuzulu kwa waziri huyo mnamo Aprili 2008, baada ya miezi minne tu ofisini. [9]
Moreno alijitenga na mke wake Amelia aliempatia watoto wawili ambao ni Joseph Paul na Victoria.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ^ a b c d e Diario Perfil: Guillermo Moreno: Biografía no autorizada del apretador oficial de los K, Archived 21 Julai 2009 at the Wayback Machine. 20 Aprili 2008.Lugha ya Kihispania
- ^ Clarín: La carne no bajó y Kirchner decidió cambiar a uno de los negociadores, Archived 20 Aprili 2006 at the Wayback Machine. 13 Aprili 2006.Lugha ya Kihispania
- ^ La Nación Online: Fuerte y amplio rechazo a la defensa oficial de Guillermo Moreno Archived 7 Septemba 2008 at the Wayback Machine., 30 Julai 2008.Lugha ya Kihispania
- ^ Periodismo de Verdad: El matrimonio Kirchner decide si Guillermo Moreno y Ricardo Jaime continúan en sus cargos, Archived 18 Agosti 2022 at the Wayback Machine. 15 Mei 2008.Lugha ya Kihispania