Gina Ahadi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Gina Ahadi (amezaliwa 2 Mei 1999) ni mwanamitindo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mkongo wa kwanza kushinda Tuzo ya Miss Global.[1] Mnamo 3 Mei 2021 alishindana katika kinyang'anyiro cha Miss Kentucky, Marekani, lakini hakushinda, hivyo akatunukiwa taji la Miss Global.

Miongoni mwa vitu alivyovifanya mwanamitindo huyo ni pamoja na matukio anayofanya katika jamii yake ikiwemo matukio ya kusaidia watoto na watu wasiojiweza.

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Gina alizaliwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Alihamia Uganda alipokuwa mdogo ambapo wazazi wake walikuwawakiishi kama wakimbizi. Walikaa Kampala Uganda kwa takriban miaka 8 ambapo wakati huo Gina alikuwa akisoma shule ya msingi. Mnamo 2004 Gina na familia yake walihamia marekani USA, alianza shule ya kati ama sekondari na kuhitimu na GPA ya 4.0. Pia alienda shule ya upili ama kidato cha tano na sita ambapo alihitimu pia na kiwango kile cha uwezo wa GPA 4.0 ,kisha akatuma maombi kwenye Shule ya matibabu na kufuzu kama Msaidizi wa Matibabu.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Gina anafanya kazi kwenye kituo cha walezi wa watu wazima huko marekani. Mnamo mwaka 2018 Gina alianza kujihusisha na kazi aliyotokea kuipenda ya uanamitindo, alianza kwa kupiga picha za kawaida, ambapo picha zake zilikuwa zikivuma sana na watu kuzipenda kwakua ndizo picha zilizokuwa zikionekana za mwanamke kutoka nchini Kongo huko Marekani akipiga picha akiwa amevalia bikini. Alianza hivyo na kuonekana sana katika video nyingi za muziki na wasanii mashuhuri kama vile Unanifaa ya Destin na Rich da Chris, Congo ya Mandi classic  na Salima ya snazzy.

Mnamo mwaka 2019 miss fashion Global ilimfikia na kumuomba ashiriki katika shindano lao kama mwanamitindo[2]. Gina alihudhuria na kushindana lakini hakushinda pia hakufika fainali. Zaidi pia alliomba kushiriki shindano la miss houston USA lakini hakufanikiwa kutokana na vipimo vya ugonjwa wa uviko 19 kuonyesha ana ugonjwa huo, na hivyo kuwekwa kando na shindano hilo, na kwa hivyo hakupata nafasi ya kushiriki katika shindano hilo. Lakini katika mwaka huo huo aligombania nafasi ya kushiriki tena katika shindano la Miss Global kwa mwaka wa 2021 na wakati huu alifanikiwa kufika fainali na kutwa mshindi nafasi ya pili.[3] Pia Gina ni mshiriki wa shindano la The Fashion hero [4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Miss Global Contestants". Miss Global Organization (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2022-08-08. 
  2. "Vote for Gina ahadi in the MFG Photo Contest.". GoGo Photo Contest (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-08-08. 
  3. "Miss Global Contestants". Miss Global Organization (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2022-08-08. 
  4. The Fashion Hero (2022-08-09). "Gina Ahadi | USA". www.thefashionhero.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-08-09. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gina Ahadi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.