Gerty Cori

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gerty Theresa Cori mnamo mwaka 1947

Gerty Theresa Cori (15 Agosti 1896 – 26 Oktoba 1957) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ucheki.

Baada ya kufunga ndoa na mumewe Carl Cori mwaka wa 1920, walihamia Marekani na kupata uraia wa huko mwaka 1922.

Pamoja na Carl alichunguza umetaboli wa kabohaidreti katika kiumbehai cha wanyama.

Mwaka wa 1947, pamoja na mumewe Carl na Bernardo Houssay alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.

Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gerty Cori kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.