Nenda kwa yaliyomo

George Lucas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
George Lucas

George Lucas, mnamo 2009.
Amezaliwa George Walton Lucas, Jr.
Mei 14 1944 (1944-05-14) (umri 80)
Modesto, California, Marekani
Kazi yake Mwongozaji, mtayarishaji
Miaka ya kazi 1965-hadi leo
Ndoa Marcia Griffin (1969-1983)
Mellody Hobson (2013)
Watoto 4

George Walton Lucas, Jr. (amezaliwa tar. 14 Mei 1944 mjini Modesto, California) ni mwongozaji, mtayarishaji na mwandikaji wa script wa filamu wa Kimarekani. Huenda akawa anafahamika zaidi kwa kutayarisha mfululizo wa filamu za Star Wars na mfululizo wa filamu za Indiana Jones.

Lucas pia aliongoza filamu za THX 1138 (1970) na American Graffiti (1973). Akiwa pamoja na rafiki yake wa karibu Bw. Steven Spielberg, walifanikisha kutengenezwa kwa mfululizo wa filamu za Indiana Jones. Lucas vilevile ni mtaalam wa kuweka vionjo mbalimbali vya bunilizi ya kisayansi, na pia ameanzisha kampuni yake inayoandaa mambo mengi yahusianayo na filamu na kadharika. Alikuwa mwandishi sugu na aliyeshamiri katika uwanja wa uigizaji (sonkolimike@gmail.com).

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu George Lucas kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.