George Cleopa Mapunjo
George Cleopa Mapunjo Mpembeni (alizaliwa tarehe 28 Septemba 1980 katika Wilaya ya Malinyi, Mkoa wa Morogoro.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Ni mzaliwa wa kwanza katika familia ya Mzee Cleopa Elinisafi Mapunjo Mpembeni wa Wilaya ya Same iliyopo katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Alipata elimu yake ya Msingi katika Shule ya Makugira na Mwembeni kabla ya kuja Dar es Salaam na kujiunga Shule ya Msingi Ilala Kasulu Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam na kumaliza mwaka 1995.
Kisha aliendelea na masomo yake ya Sekondari katika Shule ya Sekondari ya Kibasila alikosoma kwa miezi mitatu na kisha Pugu na Jitegemee alikomaliza kidato cha nne.
Aliendelea na masomo ya masomo ya kidato cha tano katika Shule aliyochaguliwa ya Minaki mchupeuo WA PCB lakini hakuweza kuendelea zaidi baadae alijiunga na Shule ya Sekondari ya Aga Khan Mzizima kwa mchupuo huo wa Sayansi Lakini aliushindwa na kuamua kubadilisha mchepuo na kusoma HKL katika Shule ya Sekondari St Mary's Jiji Dar es Salaam na kumaliza mwaka 2006.
Mwaka huohuo 2006 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kusomea kozi ya Ualimu katika masomo ya Kiswahili na Historia.
Alipomaliza Chuo, 2009,aliajiriwa Serikalini kama Mwalimu wa Sekondari Jijini Dar es Salaam na kituo chake cha kwanza cha kazi ni Benjamin William Mkapa High School.
Mwaka 2012 alijiunga kusomea shahada yake ya pili, shahada ya Uzamili wa fasihi ya Kiswahili (M.A. Kiswahili) na kumaliza mwaka 2014 Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Aliona hakutosheka na elimu, mwaka 2015 alijiunga kuendelea na masomo ya Uzamivu (PhD katika fasihi ya Kiswahili,anayoendelea mpaka sasa.
Utunzi wa vitabu
[hariri | hariri chanzo]George Cleopa Mapunjo Mpembeni ni mtunzi wa vitabu wa fasihi ya Kiswahili. Mpaka sasa amefanikiwa kuchapisha vitabu vitatu, ambavyo ni
- Siri ya Mtoto Ajuaye Mama (Tamthiliya) 2014
- Pasua Kichwa (Ushairi) 2016
- Tujipange watupange(Ushairi)2016.
Pia ana miswada kadhaa, ikiwemo
- Mtoto wa Mtawala(Tamthilia)
- Kiu ya Mabadiliko (Tamthilia).
George Cleopa Mapunjo Mpembeni pia ni mwandishi wa makala za lugha ya Kiswahili, Usalama barabarani, elimu ya dini na nyingine za kijamii katika gazeti la Tanzania Daima. Kutokana na uandishi huo wa makala, imempelekea kuingia kwenye shindano la jinsia kutokana kuandika makala inayolenga kutetea haki za wanawake. Shindano lilidhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na kutetea wanawake (UN - WOMEN).
Vilevile ni mwanzilishi wa kurasa jukwaa la mapunjo (mapunjo forum), kundi la anza nasi BWANA, HOJA YANGU na Chome family zilizopo facebook na WatsApp.
Mbali na utunzi, pia ni mshauri na mhamasishaji katika wa mambo mbalimbali kuhusu utetezi wa haki za binadamu. Kwa sasa anaishi jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu George Cleopa Mapunjo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |