Gelawdewos

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Gelawdewos (takriban 1521 au 152223 Machi 1559) alikuwa mfalme mkuu wa Uhabeshi kuanzia tarehe 3 Septemba 1540 hadi kifo chake. Alimfuata Dawit II.

Jina lake la kutawala lilikuwa Asnaf Sagad I. Utawala wake ulisumbuliwa hasa na vita. Kwanza alimpiga vita Ahmad ibn Ibrahim al-Ghazi aliyeshindwa na kufa katika mapigano yaliyofanyika mahali pa Wayna Daga, 21 Februari 1543. Halafu alimpiga vita Nur ibn Mujahid aliyevamia Uhabeshi. Kuanzia mwaka wa 1557 Waturuki walipotwaa mji wa Massawa Gelawdewos alipata shida sana. Aliuawa katika mapigano dhidi ya Nur. Aliyemfuata ni Menas.

Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Uhabeshi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gelawdewos kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.