Gabriel Martinelli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Martinelli akichezea Arsenal mnamo 2020

Gabriel Teodoro Martinelli Silva (anajulikana kama Gabriel Martinelli, alizaliwa 18 Juni 2001 [1]) ni mchezaji wa soka wa nchini Brazil ambaye anacheza kama mshambuliaji katika klabu ya Ligi kuu Uingereza Arsenal FC na timu ya taifa ya Brazil.

Martinelli alizaliwa na kukulia huko Guarulhos, alianza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya wakubwa akiichezea timu ya Ituano na akasajiliwa na Arsenal Julai 2019, akiwa na umri wa miaka 18. Alishinda Kombe la FA katika mechi yake ya kwanza kama mchezaji wa Arsenal.

Kazi ya mpira[hariri | hariri chanzo]

Ituano[hariri | hariri chanzo]

Martinelli alianza kazi mnamo 2010, akichezea timu ya Corinthians' futsal team. Baada ya kufanya vyema katika nyanja za soka, alihamia Ituano mwaka 2015[2] , baada ya kufanya majaribio katika klabu za Manchester United na Barcelona. Martinelli alifunga bao lake la kwanza akiwa mchezaji wa kulipwa mnamo tarehe 8 Septemba 2018, akifunga la goli la pili katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Taboão da Serra, katika mashindano ua Copa Paulista ya mwaka huo.[3]

Arsenal[hariri | hariri chanzo]

Martinelli aliripotiwa kuhitajika na baadhi ya vilabu kadhaa lakini alisaini mkataba wa muda mrefu na klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Arsenal mnamo tarehe 2 Julai 2019, kwa ada iliyoripotiwa ya paundi milioni 6 ($ 46.9 milioni). Martinelli alicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya Uingereza, tarehe 11 Agosti 2019 katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Newcastle United, akiingia dakika ya 84 akichukua nafasi ya Henrikh Mkhitaryan. Mnamo tarehe 5 Agosti 2022, Martinelli aliifungia Arsenal katika ushindi wao wa 2-0 ugenini dhidi ya Crystal Palace, na kuwa Mbrazil wa kwanza kufunga bao la ufunguzi wa msimu katika kampeni ya Ligi Kuu ya Uingereza, Mnamo tarehe 3 Februari 2023, Martinelli alisaini mkataba mpya wa muda mrefu na kilabu. Mkataba huo ulikuwa wa miaka minne na nusu, ukimunganisha na klabu hiyo hadi 2027.[4][5]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gabriel Martinelli kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.