Fumbwe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fumbwe
Dume la Fumbwe mkia-mrefu (manyoya ya majira ya kuzaa)
Dume la Fumbwe mkia-mrefu (manyoya ya majira ya kuzaa)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Viduidae (Ndege walio na mnasaba na fumbwe)
Cabanis, 1841
Jenasi: Vidua
Stresemann, 1914
Ngazi za chini

Spishi 19:

Fumbwe ni ndege wadogo wa jenasi Vidua katika familia Viduidae ambao wanatokea Afrika tu. Spishi bila mkia mrefu na yenye rangi ya nili wanaitwa kinili pia. Wakati wa kuzaa madume wana rangi ya nyeusi na nyeupe na pengine rangi nyingine au rangi ya nili tu, na spishi kadhaa zina mkia mrefu. Lakini wakati wengine wana rangi za majike, kahawia na nyeupe, wenye michirizi miwili kwa utosi, na mkia wao una urefu wa kawaida. Hula mbegu za manyasi hasa lakini wadudu pia, kumbikumbi aghalabu.

Ndege hawa hawajengi tago lao lenyewe lakini huyataga mayai yao katika matago ya ndege wa familia Estrildidae (udusio wa kiota, Kiing. brood parasitism). Kila spishi inadusia spishi yake ya Estrildidae. Vinili wadusia mitolondo, mshigi tombo au mshigi kidari-machungwa, na fumbwe wengine wadusia tunguridi, tunguhina au mishigi mbalimbali. Kinyume na kekeo fumbwe hawaharibu mayai ya mwenye tago. Huyataga mayai 2-4 kwa kuzidi yaliyomo. Mayai ya fumbwe ni meupe kama yale ya mwenyeji lakini wakubwa zaidi. Ndani ya domo la makinda inafanana na ile ya makinda ya mwenyeji na dume anaiga wimbo wake.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]